Change is here! We are now Fin Tanzania (formerly Fikia Finance).

Kiapo cha Mkopaji

1. KIAPO CHA MKOPAJI

Mimi mkopaji, naapa na kukubali kuwa:

a) Nimeona mtiririko wa taaarifa katika fomu hii kinachoonesha taarifa kamili kuhusu malipo

yote ninayotakiwa kufanya endapo nitapatiwa mkopo, na zinafanana na zile nilizooneshwa

kabla ya kusaini makubaliano;

b) Ninaelewa vigezo vya makubaliano kama nilivyoelezewa katika lugha ya Kiswahili, pamoja

na athari za mkopo uliopendekezwa;

c) Nimesoma makubaliano, au nimesomewa makubaliano;

d) Pale ambapo makato yatapitishwa kutoka kwenye mshahara wangu, natambua kuwa siwezi

kusitisha makato hayo kwa maamuzi yangu mwenyewe mpaka pale deni litapokuwa

limelipwa kiukamilifu;

e) Nimepatiwa nakala ya makubaliano haya, pia

f) Nimeelezewa taratibu za kutoa malalamiko.

g) Ikiwa mteja ataondoa maombi baada ya mchakato kuanza, mteja atawajibika kwa gharama

zilizopatikana.

2. KIBALI KUTOKA KWA MKOPAJI

Mimi mkopaji, nampa mkopeshaji ruhusa ya:

a) Kuwasiliana na mtu yeyote kuhakiki kuwa taarifa nilizompatia (mkopeshaji) katika

makubaliano, sera au mahali pengine ziko sahihi;

b) Kupata taarifa kutoka mahali popote kuhusu hali yangu ya kifedha na taarifa za benki,

Pamoja na historia ya mikopo na malipo;

c) Kutoa taarifa za mkopo huu mahali popote , ikiwemo taasisi ya taarifa za mikopo;

d) Kuhamisha mamlaka na shughuli zake tajwa katika makubaliano haya kwenda kwa mtu au

ofisi yoyote;

e) Ambapo udanganyifu umefanyika katika maombi/makubaliano haya, toa taarifa husika kwa

jeshi la polisi la Tanzania au mamlaka husika.

f) Ninatoa idhini kwa mkopeshaji (FIKIA FINANCE LTD) kutumia taarifa zitokazo katika taasisi

ya utunzaji na uchakataji wa taarifa za mikopo (CREDIT REFERENCE BUREAU) chini ya

kanuni za benki kuu ya Tanzaniana, pia kwa taratibu za mamlaka hiyo zitumike katika

mchakato wa kunipatia mkopo na pia kurudisha taarifa hizo katika taasisi ya utunzaji na

uchakataji wa taarifa za mikopo kwa ajili ya utunzaji wa taarifa hizo kisheria.

g) Ninaelewa na ninaidhinisha makubaliano niliyoingia kimkataba na mkopeshaji kuwa

h) Taarifa hizi zitaendelea kutumika na mamlaka husika hata baada ya muda wa mkopo

kuzingatia sheria na kanuni za utoaji wa taarifa husika

3. UHALALI WA MKATABA

a) Makubaliano haya hayatoweza kuvunjwa kwa namna yoyote ile ndani ya kipindi cha mkopo

kati ya mimi mkopaji na mkopeshaji isipokuwa tu pale kipindi cha mkopo kitapofikia

mwisho.

b) Makubaliano haya yataendelea kutumika kwa maombi yote ya mkopo nitayofanya kwa

FIKIA FINANCE LIMITED au nitakapohusika katika mkopo huo kama mkopaji au mdhamini.

Na pia kwa ajili ya kusaidia maamuzi ya kunisogezea kipindi cha malipo ya mkopo

nitakaopewa na FIKIA FINANCE LIMITED

4. MABADILIKO YA MAKUBALIANO

a) Makubaliano haya ni moja ya makubaliano kati ya mkopaji na mkopeshaji na mabadiliko

yatatakiwa kuwa katika maandishi na kusainiwa na mkopaji pamoja na mkopeshaji.

b) Baada ya mkopaji kupatiwa kiasi chote cha mkopo, kulingana na uchaguzi wa mkopaji katika

, mkopaji atadaiwa na mkopeshaji kiasi chote kilichopo kwenye makubaliano haya kulingana

na fomu hii.

c) Kiasi kizima cha mkopo uliokubaliwa kinatakiwa kurejeshwa katika vifungu vinavyolingana

Kulingana na fomu hii.Mkopaji hatoruhusiwa kufanya malipo ya pesa taslimu kwa

muajiriwa, wakala au afisa masoko wa mkopeshaji (hii ni Pamoja

d) Mkopeshaji hawajibiki kwa malipo hayo na anadhibitisha kuwa malipo yote yanatakiwa

kufanyika moja kwa moja kwenye akaunti ya benki ya mkopeshajii

e) Malipo yatatumika kumpunguzia mkopaji jukumu katika mpangilio ufatao;

i.Gharama za kisheria;

ii.Gharama za nyongeza/ riba ya kushindwa kulipa;

iii.Gharama kamili za mkopo; Pamoja na;

iv.Salio la mkopo aliopatiwa mkopaji.

5. MALIPO YA MAPEMA

a) Mkopaji ana haki ya kulipa kiasi chote cha mkopo ndani ya siku tatu za kazi bila kuingia

gharama yoyote, ili mradi malipo hayo yanafanywa kwenye akaunti ya benki ya mkopeshaji.

b) Kufuatia fomu hii, ada ya mchakato haitarejeshwa kwa mkopaji endapo atakamilisha malipo

yake mapema.

i.Mkopaji anaweza kulipa kiasi cha mkopo ambao bado anadaiwa katika makubaliano

haya tarehe yoyote aliyopangiwa kufanya malipo, au mara moja katika mwezi wowote

bila faini yoyote.

ii.Mkopaji anaweza kumaliza malipo yaliyokubaliwa mapema zaidi kwa kulipa kiasi chote

anachotakiwa kulipa.

iii. Kiasi kinachotakiwa kulipwa ni jumla ya malipo yafuatayo:

a. Salio la mkopo ambalo bado halijalipwa mpaka tarehe ya mwisho wa

makubaliano; pia

b. Kiasi cha riba na tozo/ malipo mengine yote ambayo mkopaji anatakiwa kumlipa

mkopeshaji mpaka hapo anapokamilisha malipo ya mapema.

iv.Kupata kiasi sahihi cha kulipa, mkopaji anakubali kupata taarifa ya malipo hayo

kutoka kwa mkopeshaji.
6.KUSHINDWA KULIPA DENI NA HATUA ZITAKAZOCHUKULIWA.

a)Mkopeshaji anaweza kuomba malipo ya deni lililobakia ndani ya muda mfupi endapo mkopaji:

i.Atakwenda kinyume na makubaliano haya au atafilisika:

a.Atakufa au atapata ulemavu wa kudumu;

b.Alitoa utambulisho wa uongo alipokuwa akiomba mkopo;

c.Atafanya kitu chochote kinachoweza kuhatarisha haki ya mkopeshaji kulingana na mkataba huu; pia

d.Akipoteza ajira yake mahali ambapo makato yake ya mkopo yalikuwa yakipunguzwa kutoka kwenye mshahara wake.

b)Mkopeshaji hatopoteza haki zake nyingine za kisheria Kwa kutumia haki yake ya kudai malipo ya mkopo kwa haraka.

c)Mkopaji anakubali kwamba, endapo mkopeshaji ameingia gharama za kisheria kutimiza makubaliano haya, mkopaji atawajibika kufanya malipo hayo ya kisheria.

d)Mkopaji anamruhusu mkopeshaji kutumia njia mbalimbali kufuatilia malipo ikiwemo kutangaza kwenye vyombo vya habari.
7. MAOMBI NA KUIDHINISHA/ KUKATALIWA

a) Mkopaji huomba mkopo kwa kujaza na kusaini makubaliano haya/ mkataba huu.

b) Mkopeshaji atakapoidhinisha na kutoa mkopo, Fomu hii vitakuwa mkataba wa

kisheria kati ya Fikia Finance na mkopaji.

c) Mkopeshaji atampatia mkopaji sababu za mambo yafuatayo katika maandishi pale

mkopaji atapohitaji;

i.Kukataa kuingia makubaliano ya mkopo na mkopaji; pia kubadili vigezo na

masharti ya mkopo ulioombwa na mkopaji.

8. UTOAJI WA MKOPO NA KURIDHIA

a) Mkopo utalipwa/utatumwa kwenye akaunti ya benki iliyooneshwa kwenye fomu hii.

b) Mkopaji anakubali kuwa mkopeshaji hatowajibika kwa uharbifu/upotevu wowote

utakaosababishwa na malipo katika akaunti iliyochaguliwa.

c) Kama malipo hayajafanyika ndani ya siku tatu za kazi, mkopaji atawasiliana na

mkopeshaji na kuonesha Ushahidi wa kutopokea malipo hayo, mkopaji anaweza

kughairisha kuchukua mkopo.

9. RIBA

a) Riba itakayolipwa kwenye mkopo itakuwa ya kiwango cha kudumu, itahesabiwa na

kuongezwa juu ya malipo ya kipindi chote kulingana na ratiba ya malipo.

b) Endapo mkopaji atashindwa kufanya malipo ndani ya tarehe iliyoubaliwa au endapo

mkopeshaji atasogeza muda wa malipo, riba ya mkopo unaodaiwa itajumuishwa na

kuwa sehemu ya mkopo kwa mwezi unaofuata. Riba iliyokubaliwa hapo awali

itatozwa juu ya jumla mpya ya mkopo.

c) Itakapomlazimu mkopeshaji kuchukua hatua za kisheria ili kupata malipo ya mkopo,

malipo yatatakiwa kuongezewa riba ya kiwango cha kudumu kama ilivyo katika fomu

hii.

d) Iwapo mkopo utachelewa kulipwa, mkopaji atatozwa 5% kwa kila mwezi

aliochelewa juu ya makato katika makubaliano haya. Tozo hiyo itatozwa baada ya

mkopaji kushindwa kulipa siku 5 (tano) baada ya tarehe ya malipo .

10. BIMA YA MAISHA YA MKOPO

a) Mkopeshaji anamtaka mkopaji awe na sera ya bima ya maisha ya mkopo kwa ajili ya

kipindi kizima cha mkopo. Mkopaji alipatiwa nafasi ya kuchagua kati ya sera ya

mkopo iliyoamabatanishwa kwenye mkopo au kutoa pendekezo la bima inayokizi

vigezo.

b) Endapo mkopaji atachagua sera ya bima tofauti na ile ya mkopeshaji, sera hiyo

itatakiwa kuidhinishwa na mkopeshaji na kuwekwa chini ya mamlaka ya mkopeshaji.

c) Endapo mkopaji atachagua sera ya bima ya maisha ya mkopo iliyopendekezwa na

mkopeshaji bima ya maisha ya mkopo itatolewa na Sanlam Life Insurance (T)

Limited;

d) Mkopaji atalindwa na bima hii kwa kiasi cha mkopo katika makubaliano haya

endapo atafariki au kupata ulemavu wa kudumu;

e) Bima hii pia itamnufaisha mkopeshaji endapo mkopaji atafariki dunia, kama tu mtoa

bima (Sanlam) atapokea uthibitisho wa kuridhisha juu ya kifo cha mkopaji; pia

f) Taarifa zaidi juu ya sera hii zinapatikana kwenye fomu ya mpangilio wa bima ya

maisha ya mkopo ambayo mkopaji alipatiwa na anakili kuipokea.

11. UDADISI WA UWEZO WA KULIPA MKOPO

Kwa kutumia taarifa zitakazotolewa wakati wa kufanya uamuzi wa kutoa mkopo

pamoja na historia ya ulipaji madeni wa mkopaji, mkopeshaji atatakiwa kufikiri kama

mkopaji anakidhi vigezo vyote vya makubaliano ya mkopo.

12. NYARAKA

Cheti /Nyaraka iliyotiwa sahihi na mkurugenzi wa kampuni ya ukopeshaji inaweza

kutumika kama kielelezo cha kuonesha kiasi cha deni la mkopo husika.

13. TAARIFA ZA MKOPO

Taarifa za hali ya mkopo zitatotelea kwa mkopaji pindi zitakapohitajika na bila gharama

za ziada.
14. SHERIA

Makubaliano haya yamezingati sheria na kanuni za Jamuhuri ya Muungano wa

Tanzania

15. UTUNZAJI WA TAARIFA ZA MKOPAJI

Mkopeshaji,wafanyakazi wake na maafisa husika hawatatoa taarifa za mkopo na miamala

husika kwa mtu yeyote au taasisi yoyote isipokuwa

i.Mkopaji ametoa ruhusa kwenye makubaliano haya;

ii. Mkopaji amethibitishwa kuwa amefilisika;

iii.Taarifa hizi zitahitajika katika mahitaji/matumizi ya sheria ama kesi mahakamani

iv. Taarifa itahitajiwa na mkopeshaji mwingine ili kuangila hali ya mkopo uliopo endapo

mkopaji ataamua kuchukua mkopo katika kampuni nyingine;

v.Taarifa hii itahitajika na mamlaka nyingine kisheria; pia,

vi. Kama ni muhimu au lazima kisheria kutangaza kwa faida ya umma

16. MALALAMIKO

a) Endapo kutakuwa na malalamiko, mkopaji atatakiwa kubainisha malalamiko yake husika

kupitia barua pepe hii info@fikiafinance.co.tz

b) Mkopeshaji atashughulikia malalamiko hayo kwa haraka,

c) Malalamiko yasipofanyiwa kazi, mkopeshaji atadhihirisha hilo wa maandishi.

17. ANUANI YA MKOPAJI

a) Taarifa zote za mkopaji zitatumwa katika anuani husika kama ilivyo ahinishwa katika

kipengele”A”.

b) Taarifa hizi zitakuwa zimemfikia mkopaji ndani ya siku kumi ama chini ya hapo kama

zitatumwa kwa barua pepe.

c) Mkopaji atatakiwa kutoa taarifa mapema endapo kama ataadili anuani na atatakiwa

kubainishqa makubaliano hayo kwa maandishi

18. KIAPO NA KUKUBALI

Mimi niliyesaini hapa chini:

a) Ninathibitisha kuwa taarifa zilizotolewa ni sahihi na za kweli na nina ahidi kutoa taarifa kwa

Mkopeshaji kwa mabadiliko yatakapojitokeza siku za baadae yanayoweza kuathiri hadhi

yangu kama mteja kwa mkopeshaji

b) Nitalipa fidia kwa Mkopeshaji kwa hasara au uharibifu unaosababishwa na mimi kwa kutoa

taarifa zisizo sahihi au zenye upungufu.

c) Ninakubaliana na kanuni na masharti ya mkopo na ninakubali kuzifuata pamoja na kanuni

nyingine zitakazotumika mara kwa mara.

d) Nina uwezo wa kulipa mkopo nilioomba.

e) Ninamruhusu mkopeshaji kuhakiki taarifa zangu na kuuliza chanzo chochote pale

inapolazimu na kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wangu wa kanuni na masharti ya

mkopeshaji wa kampuni au ofisi nyingine ya mikopo kwa mujibu wa sheria, kanuni za

maadili na taratibu zilizopo.

f) Nimeelewa ya kwamba nikitoa taarifa zisizo sahihi mkopeshaji ana haki ya kukataa maombi

yangu.

g) Nimesoma na kuelewa haki na majukumu yangu kama ilivyoelezwa kwenye vigezo na

masharti.

h) Ninakubali kuendelea na mpangilio wa bima ya Maisha ya mkopo (credit life insurance) kwa

utaratibu uliopangwa na mkopeshaji.

i) Tafadhali fahamu kwamba zoezi zima la kuchukua mkopo litasimamishwa mpaka pale

uamuzi wa kubadili bima utakapokuwa umehitimitishwa.

j) Ikiwa mkopaji atasitisha maombi ya mkopo, atalazimika kulipia gharama ambazo kampuni

itakuwa imeingia hadi wakati huo wa kusitisha